WAPENZI wasomaji wetu wa Zanzibar leo, leo tunaendelea na mapishi yetu ambapo nimewatayarishia upishi wa Gulab Jamun Nyeupe (Pakistani)
Upishi huu ni maalumu sana hasa katika kubadilisha vyakula ambavyo tumevizoea, hivyo baadhi ya siku hasa za mwisho wa wiki unaweza kubadilisha mapishi tofauti tofauti.
Kwa maana hiyo nitawafahamisha namna ya mahitaji, matayarisho na namna ya kupika.
VIPIMO
Maziwa fresh – 2 L (lita)
Siki – ¼ Mug
Maji – ¼ Mug
Sukari – 1 ½ kijiko cha chai
Unga wa ngano – 1 kijiko cha chai
Unga wa semolina – 1 ½ kijiko cha supu
Baking powder – ¼ kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Chemsha maziwa mpaka yachemke.
Changanya siki na maji umimine kwenye yale maziwa yaliyochemka, maziwa yatakatika yatafanya kama mtindi halafu epua motoni
Chuja kwa chujio maji yote yatoke na wacha mpaka ipoe ukamue maji yote.
Mimina kwenye bakuli changanya na unga wa ngano na unga wa semolina na baking powder kisha ufanye viduara vidogo dogo kama shepu ya mayai.
SHIYRA (YA KUMIMINA JUU YAKE)
Sukari – 3 vikombe
maji – 2 vikombe
Chemsha motoni aacha mpaka ichemke na iwe nzito kiasi, kisha mimina vile vidonge kwenye shiyra, chemsha kwa moto mkubwa kwa muda wa dakika 20 na moto mdogo kwa dakika 20 epua tayari kwa kuliwa .