ANKARA,UTURUKI

MAKUBALIANO na ushirikiano wa Uturuki na serikali inayotambulika kimataifa ya Libya yataendelea licha ya nia ya waziri mkuu Fayez al-Sarraj kujiuzulu.

Msemaji wa rais Ibrahim Kalin alinukuliwa akisema kuwa msaada wa jeshi la Uturuki uliisaidia Serikali ya makubaliano ya kitaifa inayoongozwa na Sarraj kurudisha nyuma mashambulizi dhidi ya mji wa Tripoli yaliyofanywa na jeshi la kamanda Khalifa Haftar.

Rais Tayyip Erdogan alisema Uturuki ilifadhaishwa na tangazo la Sarraj kwamba anapanga kujitoa kutoka serikalini.

Kalin alisema msaada wa Uturuki kwa serikali ya mjini Tripoli pamoja na makubaliano yao, ambayo ni pamoja na mkataba wa usalama yaliyotiwa saini mwaka jana,utaendelea.