NA MWANDISHI WETU
JUMUIYA ya Wanawake (UWT) Mkoa wa Kaskazini Unguja, imewataka wanawake wote mkoani humo kuhakikisha kila mwanamke anasaka kura za ushindi kwa mgombea Urais wa CCM, Dk. Hussein Ali Mwinyi ,ashinde na kuwaacha midomo wazi wagombea wa upinzani
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja, Maryam Muharam Shomari, huko Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja.
Maryam alisema CCM kimeonyesha uimara na nguvu zake utaothibitika Oktoba 28, mwaka huu pale mgombea wa CCM atakapoibuka kidedea na kuingia Ikulu.
Alisema CCM kilichotokana na ASP kwa upande wa Zanzibar bado kina nguvu kubwa kisiasa, na kinaungwa mkono na wananchi kwani kimekuwa kinatimiza ahadi zake sera na kusimamia ipasavyo misingi ya amani , umoja na maendeleo.
“Upinzani ulioanzishwa mwaka 1992 hautashindana na nguvu za kisiasa zilizowekezwa tokea mwaka 1957.CCM kitaendelea kuaminiwa kwa msimamo yake imara, sera za mshikamano ,amani na umoja wakati upinzani ukijoandaa kushabilia machafuko, kutaka zifanyike ghasia mitaani na kuitishwa maandamano” Alisema Maryam.