NA NASRA MANZI

MASHINDANO ya mpira wa miguu ya Yamle Yamle Cup yaliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji ZBC yanazidi kutimua vumbi kwa kupigwa mchezo mmoja,ambao ulizikutanisha timu ya Tilalila dhidi ya Dogodogo,uliopigwa majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Magirisi Taveta.

Katika mchezo huo timu ya Tilalila ilifanikiwa kuibuka na ushindi mabao 3-0.

Mabao ya ushindi yaliwekwa wavuni na mshambuliaji Salum Waziri mnamo dakika ya 28 na dakika 33, bao la tatu liliwekwa kimiani na Salum Kisoma kwenye dakika ya 56.