NA ABDI SULEIMAN

VIJANA kisiwani hapa wametakiwa kuendelea kuwa na uvumilivu na uzalendo wa kuipenda nchi yao, hususana katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Hayo yalielezwa na Ofisa Mdhmaini Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Fatma Hamad Rajab, wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwelewa vijana juu ya utunzaji wa amani, yaliyoandaliwa na Sshirika la UNFPA.

Alisema Zanzibar na Tanzania bado zipo katika misingi ya amani,hivyo hakuna budi kuendelea kutunzwa.Akizunguzmia uongozi bora, aliwataka vijana kuhakikisha wanaendelea kuwachagua viongozi ambao wataweka mbele maslahi yao badala ya maslahi binafsi.