NA ABDI SUELIMAN
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla, amewataka Vijana Kisiwani Pemba kufahamu kwamba kama kuna tunu ya kuitunza Tanzania, basi ni amani na utulivu uliopo nchini.
Alisema amani na utulivu huo hauwezi kupatikana sehemu yoyote duniani, hali iliyopelekea Tanzania kushika nafasi mbali mbali katika suala la amani.
Mkuu huyo wa Mkoa aliyaeleza hayo, wakati alipokuwa akifungua Kongamano la Vijana kutoka Mikoa miwili ya Pemba, lililofanyika Mgogoni nje kidogo ya mji wa Chake Chake.
“Vijana ndio watunzaji wakubwa wa amani, licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu ambao hawaitakii mema Zanzibar na wanataka kuwashawishi vijana kuingia katika mkubo huo”alisema.
Aidha Mkuu huyo aliwataka vijana kuwa mstari kuunga mkono juhudi za serikali katika suala la kulinda amani, kwani pasipo na amani hakuna maendeleo yoyote yanayoweza kupatikana.
Katika hatua nyengine Mkuu huyo wa Mkoa, aliwahimiza Vijana kuwa wazalendo wananchi yao, kwa kuunga mkono mambo yote waliotakiwa kuyatekeleza, pamoja na kuendelea kubeba dhima walionayo ya kuwa wamoja, kushikamana na kufuata sheria za nchi.
Hata hivyo, aliwataka vijana kufahamu kwamba, wazanzibari hawataki vurugu bali wanahitaji suala la amani, huku akiwataka kumuunga Mkono Mgombea Urais wa Zanzibar CCM Dk.Hussein Ali Miwnyi katika uchaguzi mkuu unaofuata.
Mapema afisa mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, Fatma Hamad Rajab, alisema lengo la kongamano hilo ni kuwapa fursa vijana kuelezea matarajio yao kwa serikali ya amani ya nane (8) inayokuja.
Akiwasilisha mada ya Vijana na Uzalendo kada wa CCM Pemba Yussuf Kaiza, aliwataka vijana kuacha kutumiwa kuvuruga amani ya nchi, hivyo wanapaswa kuwa walinzi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
“Amani iliyopo sasa hakuna mtu atakae kuja kuilinda, mani ni tunu na kuhakikisha wanapiga kura na kulinda vitambulisho vyao”alisema. Kwa upande wake katibu Tawala Mkoa wa