NA ABDI SULEIMAN
MKURUGENZI SOS Zanzibar, Asha Salim Ali, amewataka vijana kuitumia mitandano ya kijamii vizuri, ili kuepuka kuingia katika mitego ambayo itawaharibia maisha yao.
Alisema iwapo vijana wataitumia mitando hiyo kwa kusoma mbinu mbali mbali za kilimo pamoja na kutafuta fursa zinazotolewa katika mitandao hiyo, basi hawatakua na muda wa kuingia katika siasa ambazo zinaweza kuwapeleka sehemu hatari.
Hayo yaliyelezwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa vijana, juu ya masuala ya ujasiriamali kutoka shehia Vitongoji, Chonga, Michenzani, Tumbe Magharibi na Tumbe Mashariki na kufanyika mjini Chake Chake.
Alifahamisha kuwa SOS ipo tayari kushirikiana na wizara ya vijana, idara ya vyama vya ushirika ili kuhakikisha vijana wanafikia malengo yao.
Ofisa Mdhamini Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Pemba, Fatma Hamad Rajab, aliwaomba vijana kuzitumia fursa zilizopo ili kujiajiri.