NA MWAJUMA JUMA

MICHUANO ya nage ya Baraza la Vijana Magharibi A yameshindwa kutoa bingwa baada ya mchezo wa fainali uliowakutanisha Six Center na Welezo kushindwa kumalizika kwa wakati.

 Mchezo huo ulichezwa kwenye viwanja vya Regeza Mwendo ambao ulilazimika kuvunjwa kutokana na timu hizo kufanya vurugu.

Waliodaiwa kuanzisha vurugu hilo ni timu ya Welezo ambao walipingana na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo, ambae alilazimika kuuvunja.

 Welezo ambao walikuwa wakiongoza kwa mabao 9-5, walikataa maamuzi ya mwamuzi kufuatia mdimaji wa timu hiyo kutishia wakati akimpiga mchezaji wa Six Center , kitendo ambacho ni kinyume na kanuni za mchezo huo.

Kufuatia vurugu hilo ndipo mwamuzi Hadia Omar alilazimika kuuvunja na kamati inayosimamia mashindano hayo kuamua zawadi ambazo zilikuwepo kwa ajili ya bingwa zigawiwe sawa kwa sawa.