PARIS, Ufaransa

MSHAMBULIAJI wa timu ya Paris Saint-Germain, Neymar de Santos, ameripotiwa kukutwa na virusi vya corona pamoja na wachezaji wengine watatu.

Hata hivyo Paris Saint-Germain ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Ufaransa na kumaliza nafasi ya pili, kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wameshindwa kuwaweka wazi wachezaji hao wengine ambao wamekutwa na virusi hivyo.

Lakini Angel Di Maria mwenye umri wa miaka 32 na Leandro Paredes mwenye miaka 26, wanatajwa kuwa kati ya wachezaji hao kwa mujibu wa L’Equipe.

Mara baada ya Paris Saint-Germain kumaliza mchezo wa mwisho wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich, Agosti 23, wachezaji hao watatu walionekana kuwa pamoja kwenye visiwa vya Ibiza wakiponda raha ambapo ni Neymar, Di Maria na Paredes.