BRASILIA, Brazil

WACHEZAJI wa timu ya taifa ya wanawake ya Brazil watalipwa posho sawa na wachezaji wa timu ya wanaume, ametangaza Rais wa shirikisho la soka Brazil CBF Rogerio Caboclo.

CBF inakuwa miongoni mwa mashirikisho machache Duniani yanayolipa posho sawa kwa timu za taifa za wanawake na wanaume, mataifa mengine yanayofanya hivyo ni Australlia, Norway na New Zealand.

Malipo haya yataanza katika michuano ya Olympic itakayofanyika mwakani na katika fainali za kombe la Dunia.

Rogerio Caboclo. Amesema ‘itakuwa sawa kwa wote kama mapendekezo ya FIFA yanavyotaka kwenye soka la wanawake, hivyo hakutakuwa na utofauti wa jinsia’.