WASHINGTON,MAREKANI

WANASIASA wa Democrat nchini Marekani wamemshambulia vikali Rais Donald Trump baada ya ripoti ya gazeti la The New York Times kusema  kwamba bilionea huyo ama alilipa kidogo sana au hakulipa kabisa kodi ya mapato katika miaka iliyopita.

Pia alikuwa akikabiliwa na kiwango kikubwa cha madeni.

Spika Nacy Pelosi wa Baraza la Wawakilishi alikiambia kituo cha televisheni cha MSNBC kwamba Wamarekani wanastahiki kujuwa wanaomdai Trump.

Spika Pelosi alisema kwamba endapo wadai ni mataifa ya kigeni, madeni hayo ni hatari kwa usalama wa taifa, kwani yanaweza kumuweka rais kwenye nafasi ya kushinikizwa.

Gazeti la The New York Times linasema kwamba mwaka 2017, Rais Trump alilipa dola 750 tu kama kodi ya mapato nchini Marekani, lakini akalipia zaidi ya dola laki tatu kwa mataifa mengine.

Trump aliikanusha ripoti hiyo akiita kuwa ni taarifa za uzushi.