KAMPALA,UGANDA

WANANCHI wa Uganda watalipa shilingi 240,000 za Uganda ($65) kwa ajili ya kipimo cha COVID-19 wakati Serikali ikisimamia gharama hizo katika hatua ya kukabiliana na janga hilo.

Waraka wa Serikali kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Geoffrey Sseremba alisema, huu ni utaratibu wa kuokoa gharama ambao utaiwezesha Wizara ya Afya kununua vifaa zaidi vya kupimia ili kuendelea kufanya huduma hii ya upimaji kufikiwa nchini kote.

Wananchi wa Uganda, hata hivo, wanahoji hatua hii, wakiwa wanatafakari kiwango kikubwa cha fedha ambazo nchi imepokea katika miezi mitano iliyopita kwa ajili ya kudhibiti virusi hivyo.

Malipo haya ni kwa yoyote anayetaka kupimwa COVID-19, lakini Serikali iliorodhesha wale ambao lazima wafanyiwe vipimo.

Walioorodheshwa ni madereva wa malori, watu binafsi wanaotaka kujua hali zao, raia wa Uganda wanaorejea kutoka nje, taasisi zinazotaka kuwapima .

Wadau wa maendeleo kama vile Shirika la Afya Duniani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa pia walichangia vifaa vya kupimia. Zaidi ya vipimo 350,000 vimefanywa kwa wananchi wa Uganda nchi nzima.