NA MARYAM SALUM
KADA wa CCM Hanuna Ibrahim Massoud, amewaomba wanawake kuwaunga mkono wagombea wanawake katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
Alisema hayo wakati akizungumza na Zanzibar Leo nyumbani kwake Chake Chake.Alisema wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi, hivyo kama watawapigia kura wanawake wenzao wanaogombea nafasi mbali mbali za uongozi, zinaweza kupungua.