BERLIN,UJERUMANI

BAADA  ya kuzuka moto katika kambi ya wakimbizi ya Moria nchini Ugiriki katika kisiwa cha Leblos maelfu ya watu wamejitokeza nchini Ujerumani wakitaka nchi hiyo kuwachukua wakimbizi ambao kambi yao imeungua moto.

Maandamano makubwa yalihudhuriwa na watu 10,000 mjini Berlin.

Kwa mujibu wa shirika la Seebridge watu 3000 walijitokeza mjini Koeln na wengine 2500 walishiriki maandamano hayo mjini Hamburg.

Katika usiku wa Jumatano mto ulizuka katika kambi ya wakimbizi ya Moria,na kuharibu kambi yote.

Usiku katika eneo ambalo liliharibiwa kiasi na moto katika kambi hiyo, moto mwengine ulizuka wakati wahamiaji wakishughulika kutengeneza mahema yao.