NA MWANAJUMA MMANGA

JESHI la polisi Mkoa wa Kusini Unguja limewashikilia vijana wawili kwa tuhuma ya makosa tofauti huko mkoa wa Kusini Unguja.

Kamanda wa polisi wa Mkoa huo, Suleima Hassan Suleima, akithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja vijana hao ni Kipe Mussa Makame (25) mkaazi wa Jambiani kwa kosa la kupatikana na pombe ya kienyeji (Gongo)katika gari huko Paje, na Rashid Ali Mohammed (25) mkaazi wa Jambiani amekamatwa na nyongo 112 pamoja na furushi moja la majani makavu lenye uzito wa gram 200 yanayosadikiwa kuna bangi.

Alisema kijana Kipe alipatiokana na ulevi huo katika gari ya abiria akiwa na chupa 24 zenye ujazo wa lita moja na nusu zikiwa zimejaa ulevi  hapo mbele ya kituo cha polisi Paje.

Alisema tukio hilo limetokea Septemba 18 mwaka huu majira ya saa 12 jioni huko Paje mbele ya kituo cha polisi kijana huyo alipatikana na ulevi wa gongo katika gari wakati ikiwa inasachiwa mizigo hapo kituoni yenye ruti namba 309 ya Jambiani ambapo namba za usajili hazijafahamika

Aidha Suleiman alisema kijana Rashid alipatikana akiwa na furushi hilo alilokuwa amelivunga katika gazeti la kichina na kuhifadhi ndani ya mkobawa rasketi nyeusi aliokuwa ameuvaa shingoni mwake tukio hilo limetokea Septemba 19, mwaka huu majira ya saa 11 za jioni huko Jambiani.