NA FATMA AYOUB, MCC

WAKULIMA na wauzaji wa mazao ya viungo vya mchuzi wametakiwa kutokata tamaa katika kulima na kuuza mazao hayo kufuatia kushuka kwa bei ya bidhaa hizo.

Kauli hiyo imetolewa na mmoja kati ya wakulima wa kilimo hicho, Ali Said Ali, alipokuwa akizungumza na gazeti hili huko Sokoni Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi ‘B’ Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Alisema kuwa wakulima wasikate tamaa kwani ndiyo kawaida ya biashara kuna siku itapanda na siku itashuka na mazao yaliyo shuka bei  ni pamoja na Tungule, Pilipili boga, Vitinguu maji, mbatata na keroti,

Akitaja bei za bidhaa hizo ikiwemo tungule ilikuwa kilo shilingi 3000 kwasasa kilo shilingi 1000 hadi 500, mbatata kilo ilikuwa 2500 na kwa sasa kilo 700 Pilipili ilikuwa kilo 3000 kwas asa kilo moja shilingi 500

Alisema hayo yametokea kufuati watu wengi wamekuwa wakilima bidhaa hizo na maneo ya kuzia ni machache, jambo ambalo limewarudisha nyuma baadhi wakulima na wauzaji hasa hasa wale wa bidhaa ya Pilipili boga.