KUPOTEZA fahamu kutokana na unywaji wa pombe kupita kiasi ni hali ambayo watu wengi wenye kunywa kinywaji hicho wameshawahi kukumbana nayo japo mara moja katika maisha yao.

Suala la kusahau au kupoteza kumbu kumbu baada ya kunywa pombe nyingi limezua gumzo nchini Marekani kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili jaji Brett Kavanaugh aliyeteuliwa na rais Trump.

Mmoja wa wale wanaomtuhumu jaji Kavanaugh, anadai kuwa alimnyanyasa kingono akiwa mlevi zaidi ya miaka 36 aliyopita.

Mwanamke mwingine anadai kuwa jaji huyu alijitupa kwake akiwa amelewa chakari wakati wa michezo wakiwa chuoni.

Hata hivyo, jaji Kavanaugh amekanusha madai hayo huku baadhi ya watu wakisema huenda alipoteza fahamu kutokana na ulevi kupindukia japo amepinga uwezekano wa kupoteza kumbukumbu wakati alipokuwa akielewa sana.

Kupoteza fahamu kutokana na unyaji wa pombe kunatokana na hali ya ubongo kushindwa kunakili kumbukumbu za mambo yanayofanyika katika mazingira ya mtu anapokua mlevi.

Kwa mujibu wa taasisi ya kitaifa ya kukabiliana na matumizi mabaya ya vileo, hali hiyo hutokea kwa sababu mzunguko katika eneo la ubongo wenye jukumu muhimu la kuimarisha kumbukumbu za maisha ya kila siku, imefungwa na pombe.

Mtaalamu wa sayansi ya tabia ya watu katika jamii kutoka Chuo Kikuu cha Brown huko Providence, Rhode Island, Prof. Kate Carey alisema upo uwezekano mkubwa wa mtu kupoteza kumbukumbu pale anapokuwa kwenye hali ya ulevi.

“Kati ya asilimia 30 na asilimia 50 ya vijana ambao wanakunywa pombe wameripoti hali ya kupoteza fahamu na kutojua wanayoyafanya wakati wakiwa kwenye hali ya ulevi”, alisema Prof. Kate Carey,

Mtaalamu huyo alibainisha kuwa utafiti umebainisha kuwa watu walio na miili midogo hukabiliwa na hatari kubwa kutokezawa na hali ya kupoteza fahamu hasa wanapokunywa pombe kupindukia.

Wanawake pia hukabiliwa na hali hiyo kwa sababu viwango vya pombe hupanda haraka kwa wanawake kadiri wanavyokunywa pombe pasi na kunywa maji.

Geni ya mtu pia inaelezea ni kwa nini watu wengine hupoteza fahamu wanapokunywa pombe kupindukia na wengine hawajipati katika hali hiyo.

Baadhi ya wataalamu pia wanasema watu wanao vuta sigara huku wakinywa pombe wako katika hatari ya kupoteza fahamu kutokana na ulevi.

Prof. Kate Carey, alisema mtu anaweza kujieleza vizuri akiwa mlevi na hata kujua njia ya kuenda nyumbani akiwa amalewa.

Prof. Carey anasema ”Ukimuuliza mtu aliyekuwa mlevi jinsi alivyofika nyumbani hakumbuki nini kilichofanyika alipokuwa amelewa”.

Mlevi wakati mwingine huchanganyikiwa kadri kiwango cha kileo kinavyoongezeka mwilini mwake kiasi kwamba inafikia hatua hawezi kuendelea hata na mazungumzo.

Kwa mujibu wa kituo kilichopo nchini Marekani cha masuala ya ulevi na madhara yake, watu wanaweza kujiingiza katika tabia ambazo hawana wakiwa katika hali za kawaida pale wanapokuwa kwenye hali ya ulevi.

“Ukiwa mlevi, inakuwa rahisi kwako kudhulumiwa kwa njia mbalimbali. Wakati huohuo, unaweza kuhatarisha maisha ya wengine, kwa kufanya mambo ambayo usingefikiria kufanya ukiwa na akili timamu”, alisema Prof Carey.

Mara nyingi mlevi huwa hakumbuki yale yaliyojiri siku iliyotangulia alipokua amelewa chakari. Hii inatokana na hali ya yeye kupoteza fahamu zake za kawaida.

Hata hivyo hali ya kupoteza fahamu mara kwa mara mtu akinywa pombe huenda ni ishara ya tatizo la kiafya ambalo huenda likasababisha maradhi ya ini.

Habari mbaya kwa wale ambao huwa wanafurahia na kufikiri kwamba bilauri moja ya mvinyo kwa siku ni nzuri kwa kiafya.

Utafiti mkubwa uliofanywa duniani na kuchapishwa katika jarida la lancet umethibitisha kwamba utafiti uliofanywa awali na kuonyesha kwamba hakuna usalama katika unywaji wa pombe.

Watafiti wamekubali kwamba kunywa kwa kiasi kunaweza kumlinda mtu dhidi ya ugonjwa wa moyo lakini waligundua kwamba kuna hatari ya mtu kupata saratani na kukosa kinga ya magonjwa mengine.

Mwandishi wa utafiti huu alisema matokeo aliyoyapata yalikuwa muhimu sana kwa sasa kwa sababu ya mambo mengi yaliyozingatiwa

Utafiti uliofanywa na ‘Global Burden of Disease’unaangalia kiwango cha pombe na madhara yake kiafya kwa mataifa 195 ikiwemo Uingereza katika miaka ya 1996 mpaka 2016.

Utafiti uliangalia umri kuanzia miaka 15 hadi 95, mtafiti alilinganisha watu ambao wanakunywa pombe hata chupa moja kwa siku na wale ambao hawanywi kabisa.

Na kubaini kwamba watu wasiokunywa kati ya 100,000 ni watu 914 tu ndio wanasumbuliwa na matatizo ya kiafya kama saratani au kusumbuliwa na majeraha yeyote.

Lakini watu wanne zaidi wanapata madhara kama wanakunywa pombe hata chupa au bilauri moja kwa siku.

Kwa watu ambao hunywa chupa mbili za pombe kwa siku,Watu 63 kati yao uanza kupata mabadiliko ya kiafya na wale ambao hutumia chupa tano kwa kila siku kuna ongezeko kubwa la watu wapatao 338 ambao hupata madhara ya kiafya.

Kiongozi wa tafiti hiyo Dk. Max Griswold kutoka Taasisi ya Health Metrics and Evaluation (IHME) katika chuo cha Washington alisema kwamba utafiti wa awali ulibaini kwamba kuna hatari kubwa za kiafya ambazo zinahusishwa na uongezekaji wa uywaji wa pombe.

Uhusiano mkubwa wa matumizi ya pombe na hatari ya kupata saratani pamoja na magonjwa ya kuambukiza inaondoa kinga ya ugonjwa wa moyo katika utafiti.

Ingawa hatari ya matumizi ya pombe huanza polepole hukua kwa haraka kwa watu ambao hunywa pombe kwa kiwango kikubwa.

Mwaka 2016, serikali Uingereza iliweka kiwango ambacho watu wnapaswa kutumia kwa wanawake na wanaume ili kupunguza athari ya ongezeko la ugonjwa huo.