UTAMADUNI ni sehemu muhimu inayo mtambulisha na kuweza kumjua kiundani wapi anakotoka na asili yake kwa ujumla. Utamaduni una mawanda mapana ikiwemmavazi, aina za vyakula n ahata lugha.

Kwa bahati nzuri sana pamoja na kwamba Tanzania na Zanzibar kuwepo kwa makabila mbalimbali kwa haraka haraka kabisa wanaungwanishwa na kitu kimoja kikubwa nayo ni lugha ya kiswahili.

Tofauti za wazanzibari za kawaida (sio zile za kisiasa) kama vile itikadi zao, rangi zao, mavazi yao zinaweza kuonekana wazi, lakini si kwenye lugha yao, kwani wote wanazungumza na kuifahamu lugha ya kiswahili.

Hapa ndipo ile dhana kwamba kiswahili kwao Zanzibar ndipo inapopata mashiko, kwani ni visiwa ambavyo hakupatikani eneo ambalo watu wake wanazungumza lugha ya kikabila pasi na kuelewa kiswahili.

Yapo maeneo kama vile Makunduchi, Tumbatu na Pemba wananchi wa maeneo hayo wanazungumza kiswahili, ambacho ni tofauti kidogo na kile kinachozungumzwa maeneo mengine yakiwemo mjini.

Waatalamu na wabobezi wa lugha ya kiswahili wanakataa kukiita kiswahili cha Makunduchi, Kitumbatu na Kipemba kuwa ni lugha za kikabila, bali wanakubaliana kwa kusema kinachozungumza huko ni lahaja ya lugha ya kiswahili.

Pamoja na hayo ukweli huwa unaishi milele na kamwe hauwezi kuchuja. Na ukweli ulipo ni kwamba kiswahili kinachozungumzwa pamoja na changamoto zilizopo hivi sasa ndio kiswahili kizuri (standard).

Wageni wengi wanaojifunza lugha hiyo nje ya Zanzibar wanapofika Zanzibar hujikuta wakiongeza uwezo wao maradufu kwani mbali ya kujifunza misamiati lakini pia hujifunza ‘tone’ za lugha hiyo.

Bila shaka kuna jitihada kubwa zimekuwa zikichukuliwa na serikali kupitia mamlaka zake katika kukikuza na kukiendelezalugha ya kiswahili, ili urithi wa lugha hii uweze kuendelea vizazi baada ya vizazi.

Katika siku za karibuni lugha hiyo imekuwa ikichupa mipaka kuingia katika mataifa mbalimbali ndani na nje ya Afrika.