NAIROBI,KENYA
MAELFU ya wanaume wa Kimasai wakiwa wamevalia mavazi ya rangi nyekundu na zambarau huku vichwa vyao vikipambwa na rangi nyekundu, juma hili wamekusanyika kwa ajili ya hafla maalumu ya kimila ya kuwaondoa katika umri wa vijana mashujaa (Moran) kuelekea uzee.
Takribani wanaume 15,000 kutoka Kenya yote na taifa jirani la Tanzania walikusanyika katika eneo la Maprasha Hills, jimboni Kaijado, umbali wa kilometa 128 kutoka Nairobi, ambapo katika hafla hiyo kutachinjwa ng’ombe 3,000, mbuzi na kondoo 30,000.
Sherehe hizo ambazo zinafanyika mara moja katika kila baada ya muongo, hufanyika katika eneo la kupendeza la miinuko.
Kenya inakadiriwa kuwa na jumla ya Wamasai milioni 1.2.