NA ABDI SULEIMAN.

TAKRIBAN hekta Milioni 12 ya misitu katika eneo la Kitropiki ya Dunia limepotea kwa moto mwaka 2018, ambapo ni sawa na kusema karibu viwanja 30 vya mpira wa miguu.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Global Forest Watch inaonyesha kupungua kwa misitu mwaka 2016 na 2017, licha ya upoteaji huo ulianza tokea mwaka 2001.

Kama tunavyojua miti katika eneo hili ni muhimu kwa makaazi ya watu ambapo pamoja na mambo mengine lakini husaidia utoaji wa chakula.

Mamilioni ya hekta za misitu imekuwa ikipotea katika karne za hivi karibuni, kutokana na shughuli za kibinaadamu ikiwemo biashara na kilimo.

Takwimu za mwaka 2018 zinaonyesha kuna utofauti katika upungufu mkubwa wa misitu kwa miaka miwili iliyopita, miti mingi imepotea kutokana na kuungua moto.

Chama cha waandishi wa habari za mazingira Tanzania (JET) kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la Marekani (USAID-Protect), chini ya mradi unaolenga kutoa elimu ya kutokomeza ukatili na ujangili kwa wanyamapori nchini.

JET kuwa mstari wa mbele kutetea masuala yote ya uhifadhi wa wanyamapori na umuhimu wa kulinda bayonuai zake ikiwemo miti.

Afisa mwandamizi kutoka taasisi ya kuzuwia na kupambana na Rushwa Tanzania, Ally Katonya, alisema waandishi wa habari wanapaswa kujikita zaidi katika masuala ya wanyamapori na kutokusahau misitu kuwa ndio chanzo kikubwa cha uingizaji wa fedha nchini.

Alisema Serikali ilitaifisha mali zenye thamani ya shilingi Bilioni 4.7, zinazotokana na mazazo ya misitu ni wazi kwamba misitu ni moja ya rasilimali muhimu katika suala zima la uhifadhi wa wanyamapori.

“Mazao ya misitu ni muhimu kwa serikali katika kuinua mapato, utunzaji wa mazingira wa wanyamapori na kuinua sekta nzima ya Utalii, kwani misitu ni kitu muhimu sana hasa kwa utalii wa wanyama pori nchini”, alisema.

“Hekta 81 za mazao mbali mbali ya mkurunge yalikamtwa na kuwasilishwa serikalini, tizama mazao hayo yalivyoteketea ni wazi kwamba miti iliteketea kwa wingi, hata hii utakataji wa miti na upigaji wa mkaa ni tatizo pia”, aliongeza.

“Misitu ni moja ya rasilimali muhimu sana inayoingiza fedha nyingi, bado watanzania tumeisahau sekta hiyo na nisekta inayopaswa kulindwa na kuhifadhiwa”amefahamisha.

Naye Afisa kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Salimu Hakim Msemo, alisema makosa ya ujangili ni miongoni mwa makosa yanapelekea utakatishaji wa fedha.

Aliwataka wanahabari kuandika habari hizo ili kupunguza masuala ya ujangili nchini, ikiwemo kesi ya malkia wa Tembo ambayo iligonga sana katika vyombo vya habari.

Alizitaja baadhi ya sheria zinazowatia hatiani majangili kuwa ni pamoja na sheria ya uhifadhi wa wanyamapori, sheria ya misitu, sheria ya hifadhi za taifa, sheria mahususi inayohusika na eneo la ngorongoro na sheria ya mazingira na sheria ya utakatishaji wa fedha.

Alizitaja sheria nyengine ni kanuni na makosa ya adhabu, sheria ya uhujumu uchumi na makosa ya kupangwa yanayoendana na mambo ya ujangili na sheria ya makosa ya adhabu.

“Hizi sheria ni kali sana sasa zimeanza kutumika na watuhumiwa kutiwa hatiani, hapa ndipo matukio ya ujangili wa wanyamapori yalipoanza kupungua itafika wakati matukio yataondoka kabisa”, alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chombo cha pamoja National Task Force Tanzania (NRT) Robert Mande, alisema mausala ya ujangili wakati mwengine yanawiyana na makosa ya kupangwa na yanahusisha watu wengi walio ndani nan je ya nchi.

Alisema tokea mwaka 2016 National Task Force Anti-poaching(NTAP) ilipoanza, wakati ambao matatizo ya ujangili yalikuwepo na kupelekea zaidi ya asilimia 60 ya wanyama kupotea ambapo zaidi ya Tembo 43,000 waliuwawa kati ya miaka 2010 hadi 2014.

“Bandari ya Dar na Zanzibar ndizo zilizokuwa zikitumika sana kusafirishia biashara hiyo, ambapo mwaka 2009-2013 zaidi ya tani 45,000 za ndovu zilisafirishwa ulimwenguni kote kutoka Tanzania”, alisema.

Aidha alisema mnamo mwaka 2013 Tanzania iliorodheshwa katika nchi nane ambazo wanyama walishafirishwa nje ya nchi na serikali kuandaa Operesheni Tokomeza na mwaka 2014 Tanzania ikandaa mkakati wa kitaifa wa Kupinga ujangili,

“Uhalifu unafanyika kimtandao, yapo maeneo kwenye uhifadhi uhalifu unafanyika, pia katika maeneo ya mjini lazima kuwe na mtandao mkubwa wa kuzuwia uhalifu”, alisema.

Kutokana na mikakati hiyo mwaka 2015 hadi 2020, walibaini watuhumiwa zaidi ya 3,000 wanaohusika na ujangili wawanyama pori, katika operesheni 360 walizozifanya katika nchi mbali mbali ikiwemo Kenya, Mozambiqi, Malawi na Unganda, huku washukiwa 2000 wakitiwa mikononi.

Mande amesema walichunguza takriban visa 300 vya wanyamapori kwa hali ya juu kwa kushirikiana na mataifa, pia waliweza kukamata vipande 14,741 vya pembe za ndovu, pamoja na kushikilia pembe 25 za vifaru na imewakamata zaidi ya wanyamapori wazima 2000, ilibaini zaidi ya bunduki 2000 na risasi 25,000 kukamata na kukamatwa zaidi ya Tania 10,000 za mbao miti.

“Kesi 914 zinazohusiana na wanyamapori zilifikishwa katika mahakama, kesi 691 zilishitakiwa na kutiwa hatiani sawa na asilimia 75%, huku washukiwa 1,600 wamefungwa jela kati ya miaka 10 na 20 na washukiwa 43 walilipa faini karibu shilingi Bilioni 2,” alisema.

Hata hivyo, alisema masuala ya ujangili ya wanyamapori yamepungua kwa asilimia 80, huku ikielezwa kamba idadi ya Tembo imeongezeka katika miaka 2018-2020 na kuleta matumaini makubwa.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha waandishi wa habari za mazingira Tanzania (JET) John Chikomo, aliwataka waandishi kuandika habari za usahihi zinazohusina na wanyama pamoja na mazingira yao.

John alisema mazingira ni kitu muhimu kwa maisha ya binaadamu na viumbe mbali mbali duniani, hivyo alisema wakati umefika sasa kwa wanahabari kuelekeza zaidi katika eneo hilo.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa JET, Dk. Ellen Otaru, alisema suala la uhifadhi wa wanyama pori lina uwanja mpana sana, kwani hata mazingira na vilivyozunguka vyote vinapaswa kuhifadhiwa.