GABORONE, BOTSWANA

WANAWAKE walioolewa kwa mara ya kwanza wanaweza kumiliki ardhi pamoja na waume zao, amesema rais wa wanchi hiyo Mokgweetsi Masisi.

Hadi sasa, sera ya ardhi ya nchi hiyo inawazuwia wake kumiliki ardhi, kama waume zao tayari wanamiliki ardhi nchini humo.

Sheria za nchi hizo zinaeeza kuwa wanawake ambao bado hawajaolewa ambao hawana ardhi ndio wanaokubaliwa kisheria kumiliki ardhi.

Ubaguzi huo uliwaacha mamilioni ya wanawake bila uwezo wa kupata ardhi katika maeneo wanamoishi na kufanyakazi.

Rais alitweet kwamba sheria iliyofanyiwa mabadiliko : “Kila Mbotswana atakuwa na uwezo wa kupata ardhi ya makazi katka eneo analochagua katika nchi, katika ardhi ya taifa nay a kikabila .”

Alisema kuwa sera mpya pia itawalinda wanane na yatima wanaoongoza familia na wanaohitaji ardhi kwa ajili ya makazi.

Makundi ya kutetea haki za binadamu wameafiki mabadiliko hayo wakisema yamechukua muda mrefu kufikiwa.