NA JAMILA ABDALLA, MAELEZO

AKINAMAMA   kisiwani Pemba wametakiwa kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kiweze kuendelea kuleta maendeleo.

Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto, Shadya Mohamed Suleiman,   wakati akizungumza na wanawake wajasiriamali na wafaidika wa mfuko wa maendeleo wa TASAF  wa kaya maskini wa shehia ya Ole Wilaya ya Chake-Chake.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya mambo mengi ya maendeleo mijini na vijiji hivyo ni vyema kuhakikisha wananchi wanajitokeza kwa wingi kukipigia kura chama hicho.

Alisema wanawake wana nguvu kubwa katika kuleta maendeleo pale wanapounganisha nguvu, hivyo aliwataka kuunganisha nguvu hizo kwa kwenda kukipigia kura chama hicho.