NA NASRA MANZI

SKULI ya Kidoti, Mkwajuni,Uzini, na Kigunda wanawake na wanaume zimefanikiwa kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya Elimu Bila ya Malipo kwa upande wa mbio za nyika, zilizofanyika jana asubuhi katika uwanja wa Mnazi mmoja.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza kutoka Kaskazini ‘A’ Mwaka Kombo Vuai wakati mshindi wa  pili Aisha Haji Vuai kutoka skuli ya  Kidoti msingi,huku  mshindi wa tatu Hajra Hussein Ramadhan kutoka skuli ya Kigunda.

Msingi wanaume mshindi ni Bilali Abdalla kutoka skuli ya  Uzini, Twalib Makame kutoka skuli ya Kilindi ,ambapo mshindi wa tatu Juma Khamis Juma kutoka skuli ya Kigunda.

Sekondari wanawake mshindi wa kwanza kutoka Kaskazini ‘A’ ni Raifat Ali Khamis kutoka skuli ya Mkwajuni,wakati mshindi wa pili Sabahi Makame kutoka skuli ya Kidoti,mshindi wa tatu  Zuhura Kombo kutoka skuli ya Kinndi Wete Pemba.

Wanaume Secondari mshindi wa kwanza kutoka Kaskazini ‘A’ Hanifa  Ilyasa Ali skuli ya Kigunda,wakati mshindi wa pili kutoka Wilaya ya Kati Adam Khamis Burhani skuli ya Kinndi ,mshindi wa tatu Ilyasa Hamadi skuli ya Mtoni Wete Pemba.