HABIBA ZARALI

OFISA wanawake na watoto wilaya ya Mkoani, Asia Abdalla Said, amewataka wanawake wilayani humo, kuacha kusuluhishana pale wanapopatwa na kesi za udhalilishaji.
Alisema katika jamii matukio ya udhalilishaji yapo mengi ambapo mara nyingi wanaoathirika ni wanawake na watoto.

Akizungumza katika mkutano wa mapambano dhidi ya udhalilishaji uliofanyika skuli ya Mizingani, alisema athari ya vitendo hivyo haibakii kwa mtoto pekee bali mpaka ndani ya familia na taifa kwa ujumla.

Alisema si jambo la busara kwa jamii kusuluhishana wenyewe kwa wenyewe katika kesi za udhalilishaji kwani kunachangia kuongezeka kwa matukio hayo.


Alieleza kuwa wapo baadhi ya wananchi bado wana uelewa mdogo kwa
baadhi ya matukio hayo na hukubali kupokea fidia, kufuta kesi kirahisi na kutojua hatua za kuchukua jambo ambalo linarejesha nyuma harakati za mapambano hayo.

Akizungumzia kuhusu kuchelewa kwa kesi hizo alisema huchangiwa na mambo mengi ikiwemo kutotolewa ushahidi, kutoroshana, muhali na kusuluhishana jambo ambalo si jema.

Alisema miongoni mwa athari za udhalilishaji wa kijinsia ni pamoja na kuharibika kwa viungo vya uzazi, kupata ulemavu, kupata maumivu makali, kupata athari za kisaikolojia na kuwa na moyo wa kulipiza kisasi  na kukosa kujiamini.

Akizitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa na serikali alisema ni kuanzisha vituo vya mkono kwa mkono kila wilaya Unguja na Pemba, kuanzisha kamati za kupambana kila shehia, wilaya, Mkoa na hata taifa.Mratibu wa mradi, Masoud Suleiman Daud, alisema
.