MINSK, BELARUS

WATU wapatao laki moja waliandamana kwenye mji mkuu wa Belarus, Kiev,kumshinikiza Rais Alexander Lukashenko aondoke madarakani, ikiwa ni siku ya 50 mfululizo kwa waandamanaji kuingia mitaani.

Maandamano hayo yalifanyika pia kwenye miji mengine tisa, yakionesha jinsi hasira dhidi ya Lukashenko zinavyozidi kusambaa.

Wizara ya mambo ya ndani ilisema kiasi watu 200 walikamatwa, Wajumbe wengi wa Baraza la Kukabidhiana Madaraka,chombo cha upinzani kinachoratibu maandamano hayo,walikamatwa ama kukimbilia nje ya nchi.

Maandamano hayo yalianza rasmi uchaguzi wa tarehe 9 Agosti, ambapo Tume ya uchaguzi ilimpa Lukashenko ushindi wa asilimia 80.

Wapinzani na baadhi ya waangalizi wa uchaguzi wanadai kuwa matokeo hayo yalichakachuliwa na hivyo kumtaka mtawala huyo aliyepachikwa jina la dikteta wa mwisho wa Ulaya ajiuzulu.

Lukashenko alikataa na wiki iliyopita aliapishwa rasmi kuendelea na muhula wake,huku Umoja wa Ulaya ukikataa kuutambuwa urais wake.