PARIS, UFARANSA

WASHUKIWA wawili kuhusiana na shambulio la kisu ambalo lilijeruhi watu wanne mapema Ijumaa karibu na ofisi za zamani za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo wamekamatwa, viliripoti vyombo vya habari vya hapa.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kitaifa ya Kupambana na Ugaidi ilitangaza kufanyika uchunguzi  wa “jaribio la mauaji kuhusiana na biashara ya kigaidi.”

Mnamo Januari 2015, shambulio la kigaidi katika ofisi za Charlie Hebdo lilisababisha watu 12 kuuawa. Katika siku zilizofuata, polisi wa kike alipigwa risasi na kuuawa na pia kulikuwa na shambulio kwenye duka kubwa la Kiyahudi. Wahusika wakuu wa mashambulio hayo waliuawa katika upekuzi wa polisi.

Mapema Septemba mwaka huu, kesi ya washukiwa 14 walioshtakiwa kuhusiana na mashambulio haya imeanza jijini Paris.