HIVI sasa ni wakati wa harakati za kugombea nafasi za uongozi wa nchi, kuanzia kwenye wadi zinazoongozwa na madiwani, majimbo yanayoongozwa na wabunge na wawakilishi na urais wa Jamhuri na wa Zanzibar.
Mchakamchaka wa kuwania nafasi hizo za uongozi umenza kwa vishindo, ambapo unatarajiwa kuhitimishwa mnamo Oktoba 28 mwaka huu kwa zoezi la uchaguzi litakalofanywa na wananchi wenye sifa za kuchagua.
Bila shaka ni haki ya kidemokrasia kwa kila Mtanzania anayejiona anazo sifa za kuwania nafasi hizo kuingia uwanjani, hata hivyo tungependa sana kuwakumbusha watia wagombea watambue kwamba cheo ni dhamana kubwa isiyotaka kufanyiwa kiburi na majivuno.
Ni wajibu wa mgombea atakayeshinda kwa nafasi aliyoomba kulinda heshima hiyo kwa manufaa ya waliomchagua, heshima yake binafsi na heshima ya nchi yake.
Kwa maana nyengine tunaweza kukizungumzia cheo ni kama kofia ambayo mtu anaweza kuivaa leo na kesho akaivua ama kumvuka na kupotea mbali, sio kwa kuchakaa, bali kwa kupokwa na waliomvisha.
Wakati mwengine masuala haya hatuna budi tuyaunganishe na tawhid kwa kueleza kuwa Mwenyezi Mungu ndiye awaaminiye watu na vyeo, wakati ambapo mamlaka za uteuzi jukumu lake ni kubariki tu.
Kwa ufahamu wetu, cheo ni mamlaka anayopewa mtu kwa ajili ya kuwahudumia wengine, hata hivyo inasikitisha pale mtu anapolewa madaraka na kuanza kutumia cheo kinyume na miongozo na matarajio ya waliompa nafasi.
Ni vyema tukakumbuka kuwa cheo sio fursa kwa ajili ya muhusika bali ni wajibu unaowekwa mabegani mwake na kukitumia kwa maslahi binafsi ni kosa kubwa na dhambi ya kiuongozi ambayo haitamwacha muhusika salama.
Tunapaswa tutambue kuwa mtu anayepewa cheo anapaswa kujilinda sana ili asiwasababishie wengine kiasi cha kuwapa maumivu na kuwatoamachozi machozi yasiyo ya lazima.
Kwa wale waliokwenye mbio za kuwania nafasi za kuchaguliwa ni vyema wakafahamu kuwa vyeo ni matunda ya msimu, hivyo mkivitumia vibaya historia ndiyo itawahukumu.
Ni muhimu pia ikaeleweka kuwa ulimwengu wa sasa sio ule wa kale ambapo raia walikuwa waitikiaji tu wa kauli na nyimbo za viongozi na wapiga kofi kwa kila walichoambiwa na wakuu wao kuitikia hewalla.
Kwa hiyo ni muhimu kwa watafuta ulwa wakakambukuka umuhimu wa kwenda na wakati kwani raia wanazidi kukomaa kidemokrasia na pia elimu ya maisha na ya kiraia zinashika kasi.
Kizazi cha sasa kimekulia zaidi katika mfumo wa utandawazi unaofanya vijana wawe wenye fikra pevu, zilizo wazi na kweli. Hawataki tena mfumo wa kuendesha mambo kwa siri.
Kwa hiyo huku viongozi wakijiandaa kufanya kampeni kuomba kuchaguliwa wajue kuwa wananchi wanaandika kila ahadi wanasubiri siku ikifika wakuulize kwa kiasi gani ahadi hizo umezitekeleza.
Cha muhimu kwa wawania uongozi kusoma alama za nyakati ili waweze kwenda sambamba na fikra za sasa, lakini wakiendelea kuwa wavivu wa kufikiri hasa ni kwa mgombea mwenye na chama chake pia