PARIS, UFARANSA

WAZIRI wa Uchumi na Fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire amesema huenda  kuwa ameambukuzwa ugonjwa wa corona.

“Nimechunguzwa na nimepatikana na ugonjwa wa COVID-19 usiku wa leo (yaani jana). Mara moja nilienda kutengwa nyumbani kwangu kwa mujibu wa kanuni za afya za serikali. Sina dalili. Nitabaki kwenye kizuizi cha faragha kwa siku 7. Ninaendelea kutekeleza majukumu yangu,” Le Maire aliandika kwenye Twitter.

Siku ya Ijumaa, watu wengine 13,215 wamepimwa na kukutwa na virusi vya COVID-19 nchini Ufaransa, na kuifanya kuwa idadi kubwa zaidi ya maambukizo yaliyorekodiwa kwa siku moja tangu kuzuka kwa coronavirus, Wakala wa Afya ya Umma nchini humo ulisema.

Ufaransa kesi zilizothibitishwa za COVID-19 kwa sasa ni 428,696 ambapo jumla ya vifo vilivyoongezeka ni 31,249, ambapo ni wastani wa ongezeko la watu 123 katika masaa 24 iliyopita na idadi kubwa zaidi ya watu wa kila siku tangu katikati ya Mei, wakati nchi ilipoanza kuregeza vizuizi.