BAMAKO,MALI
MALI imewatangaza viongozi wa Serikali mpya ya mpito katika taifa hilo la eneo la Sahel, ambao utaweza kuendeleza mahusiano madhubuti na jeshi pamoja na uwepo wa shinikizo la kimataifa la kuteuliwa kwa kiongozi baada ya mapinduzi ya kijeshi.
Katika taarifa yake ilioneshwa kwa njia ya video, kiongozi wa kijeshi Kanali, Assimi Goita alisema Waziri wa zamani wa ulinzi Bah Ndaw, atakuwa rais wa Serikali ya mpito wakati yeye mwenyewe atahudumu kama makamo wa rais.
Tangazo hilo limetolewa baada ya Jumiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi yenye mataifa 15 wanachama ECOWAS kutoa siku kadhaa kwa watawala wa kijeshi wa Mali kuwateuwa viongozi wa kiraia, ikionya kwamba haitaviondoa vikwazo vyake endapo hatua hiyo haitotekelezwa.
Vikwazo vilivyowekwa na jumuiya hiyo ni marufuku ya kibiashara na kufunga mipaka, katika kipindi ambacho kilizongwa na mapinduzi ya Agosti 18, ambayo yalimuondoa madarakani Rais Ibrahim Boubakar Keita.