NA KHAMISUU ABDALLAH

JUMLA ya ajali 16 zimeripotiwa kwa mwezi Agosti 2020 huku wilaya ya Kati ikiongoza kwa ajali nyingi kuliko wilaya nyengine kwa Zanzibar.

Mtakwimu kutoka Kitengo cha makosa ya jinai madai na jinsia Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Asha Mussa Mahfoudh alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofizi zao Mazizini Unguja.

Aidha alisema katika ajali hizo jumla ya watu wote walikuwa 41, wanawake saba na wanaumme 34 huku waliopoteza maisha walikuwa tisa akiwemo mwanammke mmoja na wanaume nane huku waliojeruhiwa walikuwa 32.

Alisema, idadi ya ajali kwa mwaka uliopita imepungua kwa asilimia 30.4 kutoka ajali 23 kwa mwezi wa Agosti mwaka 2019 hadi ajali 16 kwa mwezi huu.

Alisema, mbali ya wilaya ya Kati pia wilaya ya Kaskazini ‘B’, Magharibi ‘A’, Magharibi ‘B’, Wete na Chake Chake zimeripotiwa ajali mbili kwa kila wilaya huku wilaya ya Kaskazini ‘B’ ikiongoza kuwa na idadi kubwa ya waathiria 13 sawa na asilimia 13.   

Hata hivyo, alibainisha kuwa jumla ya makosa ya barabarani 2,121 yameripotiqwa mwezi wa Agosti 2020 ambapo makosa yote yamefanywa na wanaumme huku makosa manne kati ya makosa 10 yaliyoripotiwa yamechangia 73.1.

Alifafanua kuwa walioathirika na kupoteza maisha walikuwa ni 19 wakiwemo waenda kwa miguu 12, wapanda baskeli na pikipiki sita, madereva wanne.