NA ZAINAB ATUPAE

SHIRIKISHO la Soka Zanzibar (ZFF) limesema litaendelea kutoa elimu ya kudumisha aman, katika kipindi kizima cha kampeni na uchaguzi mkuu 2020.

Akizungumza na gazeti hili huko ofisi za ZFF hivi karibuni Rais wa Shirikisho hilo Seif Kombo Pandu,alisema hayo ni miongoni mwa majukumu yao.

Alisema watahakikisha wanafikisha elimu hiyo inawafikia wahusika wote mjini na vijini ndani ya visiwa hivyo.

Alisema elimu ambayo wanaitoa kwa wananchi hao kuwatambulisha kuwa baada ya uchaguzi kuna maisha ya baadae,hivyo wasikubali kurubuniwa kwa lengo la kuharibu amaan ya nchi yao.

“Amaan ndio jambo la muhimu uchaguzi ni jambo la kupita ambalo hufanyika siku moja,hivyo tulinde amaan yetu”alisema.

Alisema walikuwa watapita sehemu mbali mbali ikiwemo kwenye mashindano ya mpira kutoa elimu hiyo kwa wachezaji na mashabiki.

Alisema bila ya amaan hakuna jambo litakalofanyika hivyo ni vyema kuzingatia hilo katika kipindi hiki  hadi uchaguzi utakapo malizika.

Aidha aliwataka wananchi ambao wanapata elimu hiyo kuwa wafikishia wengine.

Aidha alisema wanatambua kuwa  kila mmoja anachama chake ambacho anastahiki kupigia kura,lakini  suala la amani ni jukumu la kila mmoj.