NA NASRA MANZI
ZPC Bandari imefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya timu ya Utakuja FC ya Kitope kwa kuifunga mabao 2-1.
Mchezo huo wa muendelezo wa mashindano ya soka Yamle Yamle yaliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji ZBC,lililopigwa juzi majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Magirisi Taveta.
Katika mchezo huo timu ya Bandari ilikuwa wa mwanzo kuona lango la wapinzani wao lililofungwa na Iddi Suleiman mnamo dakika ya saba.
Kuingia kwa bao hilo timu ziliimarisha ulinzi katika lango lake ,lakini katika dakika ya 32 timu ya Utakuja FC ilisawazisha bao lililowekwa wavuni na Nassor Abdalla.
Huku bao la pili la Bandari lilifungwa na Mussa Makut kwenye dakika ya 37.