MAPEMA mwaka huu nchini Guinea iliitishwa kura ya maoni ambapo ilikuwa lengo la kufuta kipengele cha ukomo wa awamu mbili za miaka mitano kila moja kwa rais kuhudumu madarakani.

Baadhi ya wananchi wa taifa hilo waliyachukulia kawaida mabadiliko hayo, lakini wapo waliokuwa na dhana na shaka kwamba rais aliyepo madarakani Alpha Condé anataka kuongeza muda wa kubakia madarakani baada ya kuingoza nchi hiyo kwa mihula miwili.

Rais Condé mzee mwenye umri wa miaka 82 ni rais wa nne wa Jamhuri ya Guinea ambapo aliingia madarakani Disemba 21 mwaka 2010 na mnamo mwaka 2015 alianza awamu ya pili.

Kutoka na kufanikiwa kubadilisha katiba na kufutwa kipengele cha ukomo wa urais, Condé ametumia nafasi hiyo kujitosa uwanjani kuwania nafasi kwa mara tatu, ambapo katiba hivi sasa sio kikwazo.

Hata hivyo, amekuwa akikabiliwa na upinzani dhidi ya mabadiliko ya katiba, ambapo watu hao wanaompinga wamekuwa wakipambana na vikosi vya usalama ambapo baadhi ya watu wameripotiwa kuuawa nchini humo.

Pamoja na ghasia na vurugu kampeni zimekuwa zikiendelea nchini humo ambapo wananchi wapatao milioni 5.4, Machi 18 mwaka huu watashuka vituoni kwenda kupiga kura kumchagua rais mpya.

Katika uchaguzi huo, endapo Condé, atashindwa kupata ushindi wa zaidi ya asilimia 50 ya kura, alazimika kuingia kwenye duru ya pili ya uchaguzi, ambapo katika uchaguzi huo anapambana na mpinzani wake wa muda mrefu, Cellou Dalein Diallo.

Kuingia madarakani kwa Condé mwezi Disemba mwaka 2010 ulikuwa mchakato wa kwanza wa demokrasia ya kweli ya kukabidhiana madaraka katika historia ya miaka 52 ya uhuru wa nchi yake.

Hali hiyo inatokana na nchi hiyo kwa muda mrefu kuwa kwenye tawala zinazoongozwa na wanajeshi ambapo wakiwa madarakani wanashutumiwa kufanya vitendo vya ukandamizaji na ukatili.

Tukio linalokumbukwa kufanywa na utawala wa wanajeshi nchini humo ni lile la mauaji ya Septemba 28 mwaka 2009, pale vikosi vilipowaua takribani wafuasi wa upinzani 160 na kuwabaka wanawake 110, waliohudhuria mkutano wa hadhara katika uwanja wa taifa.

Condé kabla ya kuingia madarakani, alitumikia kifungo baada ya kupatikana na hatia ya kumpinga jenerali Lansana Conte, ambaye alitawala nchi hiyo kuanzia mwaka 1984 hadi kifo chake mwaka 2008.

Condé, alipoingia madarakani kwa njia ya kidemokrasia alikabiliwa na kazi kubwa ya kuvifanyia mabadiliko vikosi vya usalama na kuijenga nchi katika misingi ya kidemokrasia na uwajibikaji, katika kuheshimu haki za binadamu na uwazi kwenye masuala ya fedha za umma.

Miaka 10 iliyopita imekuwa ya maendeleo makubwa kiasi katika nchini ya Guinea chini ya utawala wa Condé, ikilinganishwa na kule walikotoka wananchi wa nchi  hiyo.

Hofu ya awali ya mapinduzi ya kijeshi yanayotokea mara kwa mara nchini humo chini ya uongozi wa Condé ilianza kupungua taratibu, baada ya jeshi kufanyiwa mabadiliko na kufuatia maofisa wengi wa ngazi za juu kutakiwa kustaafu.

Timu ya mawaziri iliurejesha uchumi wa Guinea kuwa katika hali nzuri, ambapo serikali ilijenga mahusiano mazuri na shirika la fedha duniani (IMF) na jumuia za wafadhili.

Guinea ni miongoni mwa nchi zenye utajiri mkubwa barani Afrika, ikiwa na rasilimali ya madini huku serikali ya nchi hiyo ikiwa na mipango mizuri kwenye sketa ya uchimbaji wa maadini hayo.

Imani kati ya wawekezaji imerejea, ikifungua matarajio kwamba Simandou, moja wapo ya eneo lenye kifadhi kubwa ya madini ya chuma ulimwenguni.

Hifadhi ya madini ya chuma iliyonayo nchi hiyo kwa hakika inaweza kubadilisha maisha mapya kwa maelfu ya watu nchini humo.

Ikiwa ni moja kati ya nchi tatu zilizoathirika vibaya na mlipuko wa ebola, Guinea ilipata uzoefu wa kupambana na magonjwa ya kuambukiza hatimaye kupata mwanga katika mapambano dhidi ya mripuko wa ugonjwa wa corona.

Mmoja wa wazee wa siasa za kusini mwa Jangwa la Sahara, Alpha Condé alianzisha tena wasifu wa Guinea katika ramani ya kidiplomasia ya kiafrika.

Nchi ya Guinea bado inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo suala la haki za binadamu, ambapo wapinzani kama vile bwana Diallo wanakabiliwa na vitendo vya udhalilishaji.

Nchini Guinea bado yana kovu na milipuko ya mara kwa mara ya vurugu za barabarani kati ya waandamanaji wa vijana waliofadhaika na vikosi vya usalama ambavyo, licha ya mafunzo kwa mara nyingine tena, bado mara nyingi hutumia nguvu kupita kiasi ili kuzuia machafuko.

Kwa kuongezea, ahadi ya muda mrefu ya maofisa wa kijeshi kushtakiwa kwa mauaji ya Septemba 28 bado halijatekelezwa, licha ya kampeni endelevu na familia za waathirika.

Limekuwepo shindikizo la kidiplomasia kutoka nchi za kigeni kutaka mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC), iingilie kati kuwajibisha wanajeshi waliotekeleza vitendo vya kinyama ikiwa mamlaka za Guinea itashindwa kuchukua hatua.

Takriban mmoja wa wanajeshi walioshtakiwa rasmi alikuwa ameshikilia ofisi ya serikali chini ya Condé, wakati Moussa Dadis Camara, mtawala wa jeshi ambaye vikosi vyake vilifanya mauaji hayo alifanyiwa mahojiano lakini, mwishowe, aliachwa na hivi sasa anaishi uhamishoni Burkina Faso.

Kapteni Camara ameendelea kuwa na umaarufu mkubwa katika mji wa makaazi yake Guinée Forestière, na wanasiasa waandamizi wanaonekana kusita kuchukua hatua zozote ambazo zinaweza kutishia matumaini ya kupata uungwaji mkono katika eneo hilo.

Katika uchaguzi wa 2015, Diallo aliunda muungano wa ajabu wa uchaguzi na kambi yake, wakati mshirika muhimu wa kapteni Camara ni waziri mwandamizi katika serikali ya Condé.

Kuna mgawanyiko mkubwa kuhusu wa muhula wa tatu wa urais nchini humo huku uchaguzi ukikaribia, ni mpambano ndiyo yanayoshuhudiwa, ambayo yametokana na Condé wa kuwania muhula wa tatu.

Katiba mpya haijafuta mipaka ya vipindi viwili, lakini awamu za awali hazihesabiki.

Mapema mwaka huu, shirika la kikanda la ECOWAS (Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi) liligundua majina milioni 2.5 ya wapiga kura wa kubuni kwenye orodha ya wapiga kura.

Upinzani uliamua kususia kura ya maoni na kumpa njia nyeupe ya mamlaka Conde kubadilisha katiba hiyo bila ya kupingamizi bungeni.

Hivi karibuni, Condé alisema mabadiliko ya kikatiba yaliyofanywa alitamani sana kutekeleza lakini alihisi kuwa hasingeweza kuyapa kipaumbele wakati wa miaka ya mwanzo ya utawala wake.