MUNICH, Ujerumani

SIKU ya Ijumaa Hoffenheim imetoa taarifa, wachezaji wawili wameambukizwa Covid-19 na mwengine mmoja yupo karantini. Haya yamejiri mara tu baada ya kutoka kwenye mechi za Kitaifa.

Hoffenheim  jana ilitarajiwa kushuka dimbani kuchuana na Borrusia Dortmund.

Wachezaji hao wawili hawakutajwa majina yao, wamerudi kutoka katika nchi zao kushiriki  michuano ya mataifa, hata hivyo wawili hao hawakutangamana na wachezaji wengine wala wafanyakazi.

Aidha klabu ya Hoffenheim katika taarifa yake  imesema mchezaji aliye karantini ni kutokana na mmoja wa familia yake kupatika na Covid-19.

Wachezaji kadhaa wa Hoffenheim walisafiri kwa mechi za kimataifa pamoja huku Andrej Kramaric anayeichezea Croatia akiwa mfungaji bora wa ligi hiyo akiwa na mabao sita.

Kutokana na ongezeko la viwango vya maambukizo ya covid-19  Ujerumani,mechi kati ya Augsburg na  RB Leipzig jana  ilichezwa bila mashabiki uwanjani.

 Arminia Bielefeld nao watawakaribisha mabingwa watetezi Bayern Munich mbele mashabiki wasiozidi 300.

Mechi ya Borussia Moenchengladbach dhidi ya Wolfsburg ilihudhuuriwa na mashabiki 300 pekee, Freiburg dhidi ya Werder Bremen haikuwa na shabiki hata mmoja uwanjani.