NA ABOUD MAHMOUD

TAKRIBAN miaka mingi iliyopita Zanzibar ilifanikiwa kuutangaza utamaduni wake katika nchi mbali mbali duniani.

Kila ya kona ya visiwa vya Zanzibar wananchi wake wanawake na wanaume waliweza kuutangaza utamaduni wao, kupitia nyanja mbali mbali ikiwemo mavazi, vyakula na tamaduni za ngoma asilia ikiwemo taarab.

Ama kwa upande wa vyakula ilikuwa mstari wa mbele kupika vyakula vya utamaduni,pamoja na ususi wa nywele na kusuka ukili.

Kila unaemuona mitaani unatamani umuangalie kutokana na mavazi aliyovaa yanayoonyesha kwamba mtu huyo ametoka kati ya kisiwa cha Unguja au Pemba.

Vyakula

Kanzu,koti na kofia kwa akina baba na buibui la kamba kwa wanawake, waliakisi na kumtambulisha Mzanzibari kwenye mataifa mbali mbali duniani, ambapo hata mgeni anaetoka taifa jengine huvutika.

Mambo hayo yote hivi sasa yamepotea hayapo kwenye nchi yetu, kila mmoja amekua mstari wa mbele kuiga utamaduni wa mataifa mengine, jambo ambalo linaharibu mila, silka na desturi za nchi yetu.

Ule utamaduni wa mavazi haupo ambao ndio ulikua ukimtangaza Mzanzibari katika nchi yoyote anayoingia na kumfanya ajulikane anatokea wapi.

Lakini mbali na hilo kuna maswala ya vyakula, ngoma za asilia pamoja na zile silka ambazo, tulizokuwa tukizutumia kuishi na familia zetu pamoja na majirani wa karibu tumezitupa.

Hili sio jambo jema kutupa vilivyo vya kwetu ambavyo vinasaidia kuitangaza nchi, pamoja na kutuingizia kipato na kuiga vya wenzetu ni jambo la aibu sana .

Ngoma

Mbali na kuitangaza nchi lakini kutouthamini utamaduni wetu ndio unaochangia kwa kiasi kikubwa kuharibu watoto wetu na kurithisha vizazi vyetu.

Tumeshuhudia nchi mbali mbali duniani kama vile India, Nigeria pamoja na Falme za Kiarabu, zilivyokuwa mstari wa mbele kudumisha tamaduni zao katika sehemu mbali mbali.

Leo Mzanzibari anathubutu kuvaa vazi la Oman au hizo nchi nyengine na kuacha kuvaa asili ya nyumbani wakati wakiwa wanakwenda kuoa .