Aaron Wan-Bissaka
BEKI wa Manchester United, Aaron Wan-Bissaka anataka kupata tena nafasi katika kikosi cha England na atakataa kubadilisha nchi kuiwakilisha DR Congo. (Telegraph).

Mauricio Pochettino
MENEJA wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino na kocha wa sasa wa timu ya akiba ya Real Madrid, Raul wanashindania kujaza nafasi Zinedine Zidane, iwapo itatupiwa virago. (AS).

Eric Garcia
MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola ana matumaini kuwa anaweza kumshawishi mlinzi wa Hispania, Eric Garcia (19), kuongeza mkataba wake. (Independent).

Mesut Ozil
KIUNGO wa Arsenal na Ujerumani, Mesut Ozil anaweza kuhamia katika klabu ya Marekani ya MLS huku DC United ikionesha nia ya kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32. (Sun).

Donyell Malen
ARSENAL wanaangalia uwezekano wa kusaini mkataba na Donyell Malen (21), kutoka klabu ya PSV Eindhoven, miaka mitatu baada ya kumuuza mshambuliaji huyo Muholanzi kwa thamani ya pauni 540,000. (Soccernews).

Dominic Calvert-Lewin
MKATABA wa Everton wa kumsaini mshambuliaji wa England, Dominic Calvert-Lewin (23), kutoka Sheffield United mwaka 2016 ulikuwa wa bei ya chini kuliko ilivyoripotiwa kwamba alisainiwa kwa malipo ya pauni milioni 1.5, kulingana na meneja wa timu ya Toffees vijana wenye chini ya miaka 23, David Unsworth. (Sky Sports).

Joe Rodon
KLABU ya Tottenham ilishusha chini kiwango cha bei ya beki wa Wales, Joe Rodon (23), kwa pauni milioni tano baada ya kukataa kutimiza kiwango kilichotakiwa cha bei cha Swansea kulingana na tarehe ya mwisho ya EFL . (Football Insider).

Ozan Kabak
LIVERPOOL inaweza kugeuzia nia yao kwa beki wa Schalke na Uturuki, Ozan Kabak (20), huku msako wa kumtafuta mchezaji atakayeziba pengo la Virgil van Dijk (29), ukiendela. (Sport Media Set).

Sergio Reguilon
MLINZI wa Hispania, Sergio Reguilon (23), amesema, meneja wa zamani wa Real Madrid, Jose Mourinho alikuwa mtu muhimu katika kuhamia kwake Tottenham. (Sky Sports).

Florent Indalecio,
KLABU ya Newcastle wametoa ofa ya mkataba hadi mwisho wa msimu huu kwa mshambuliaji Mfaransa, Florent Indalecio (23). (Newcastle Chronicle).

Darren Fletcher
KIUNGO wa Scotland, Darren Fletcher (36), amerejea Manchester United kwa kazi ya muda ya ukocha kusaidia ukuaji wake. (Manchester Evening News).

Hakim Ziyech
Kiungo wa Chelsea raia wa Morocco, Hakim Ziyech (27), amesema fursa ya kushinda mataji kwa kucheza mchezo mzuri ilikuwa ni sababu ya yeye kuhamia Stamford Bridge. (London Evening Standard).