MUNICH, Ujerumani

SHIRIKISHO la soka nchini Ujerumani (DFB) linatumai kupata ujumbe wa wazi kutoka katika mahakama inayohusika na masuala ya michezo, baada ya matusi mazito aliyoporomoshewa nyota chipukizi wa timu ya Borussia Dortimund Youssoufa Moukoko.

Mshambuliaji wa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 19 cha Borussia Dortimund, Borussia Dortimund.

“Matusi dhidi ya Youssoufa Moukoko hayavumiliki na ni kweli kabisa haikubaliki,” rais wa shirikisho la kandanda la Ujerumani Kaskazini (NFV) Guenter Distelrath alisema wiki iliyopita.

Distelrath pia ni Makamu wa Rais wa shirikisho la soka la Ujerumani, DFB, anayehusika na mambo ya kupinga ubaguzi.

“Ningefurahi ikiwa mamlaka huru ya michezo pia itatuma ujumbe wazi, “Distelrath alisema.

Mwakilishi wa DFB Cacau pia alijibu kwa kufadhaika. “Hiyo haiwezekani. Ninalaani vikali,” aliliambia Shirika la habari dpa.

“Inasikitisha kila wakati, wakati kitu kama hiki kinatokea. Inahisi mambo kama haya yamekuwa yakitokea mara nyingi zaidi katika miaka iliyopita.

Wakati wa mchezo wa watani wa jadi chini ya umri wa miaka 19 kati ya Schalke na Dortmund Jumapili iliyopita, Moukoko alikuwa akitukanwa mara kadhaa na mashabiki wa Schalke baada ya kufunga mabao matatu.

Baada ya mechi hiyo, Schalke iliomba radhi kwa tabia ya mashabiki wake ikiwa ni pamoja na ‘hashtag ‘ya ‘Hapana Kwa Ubaguzi’ katika chapisho lao kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.