WASHINGTON, MAREKANI

WATU 60 wameuawa na kujeruhiwa kwenye matukio ya ufyatuaji risasi katika maeneo tofauti ya Marekani ndani ya masaa machache yaliyopita.

Kwa mujibu wa Kituo cha Utafiti wa Ghasia za Silaha za Moto nchini Marekani,matukio 54 ya ufyatulianaji risasi yalifanyika katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

Kwa mujibu wa kituo hicho,watu 24 waliuawa huku wengine 36 wakijeruhiwa kwenye matukio hayo.

Ripoti ya Kituo cha Utafiti wa Ghasis za Silaha za Moto nchini Marekani ilibainisha kuwa,matukio hayo yaliripotiwa katika majimbo ya Texas, Florida, Louisiana na Arkansas.

Marekani hivi sasa inashuhudia wimbi la ghasia, vitendo vya uporaji, utekaji na mashambulizi ya kutumia silaha. Maelfu ya raia wa Marekani huuawa kila mwaka katika matukio ya mashambulizi ya silaha za moto katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.

Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa, kuna silaha za moto kati milioni 270 na milioni 300 nchini Marekani, hii ikimaanisha kuwa, karibu kila Mmarekani anamiliki bunduki.

Makundi ya haki za raia yamekuwa yakitaka kuwepo sheria za kubana umiliki wa bunduki mikononi mwa raia.

Hata hivyo, Rais wa Marekani, Donald Trump anaunga mkono sheria inayoruhusu kuuzwa na kumiliki bunduki kiholela nchini humo.