NA ZUHURA JUMA, PEMBA

MAHAKAMA ya mkoa Wete imemuondolea mashitaka sita ya mashambulio ya aibu yaliyokuwa yakimkabili mzee Hamad Nassor Hamad, mwenye umri wa miaka 73 baada ya upande wa mashitaka kuchukua muda mrefu bila ya kupeleka mashahidi mahakamani.

Hakimu wa Mahakama ya mkoa Wete Abdalla Yahya Shamhun, amesema, ameliondoa shauri hilo chini ya kifungu cha 210 (2) cha Sheria nambari 7 ya mwaka 2018.

Alisema kuwa, ametumia kifungu hicho kuliondoa shauri hilo baada ya kuona kwamba ni la muda mrefu mahakamani bila kusikilizwa mashahidi.

“Shauri nimeliondoa kwa sababu ni la muda mrefu na wala halijasikilizwa mashahidi”, alisema hakimu huyo.

Kesi hiyo yenye kumbukumbu namba RM cc 23/2019 ilianza kufikishwa mahakamani mara ya kwanza Septemba mwaka jana.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mtuhumiwa huyo aliwatendea makosa ya udhalilishaji watoto hao, ambapo kosa la kwanza alilitenda siku na tarehe isiyojulikana mwaka 2018 majira ya saa 6:05 mchana eneo la Pandani Wete.

Ilidaiwa kuwa, mtuhumiwa huyo aliwaruhusu watoto wa miaka sita (6), tisa (9) na kumi (10) kubaki kwenye ukumbi wa nyumba yake kwa ajili ya kushiriki kutazama picha za ngono.