MEXICO CITY, MEXICO

WAZIRI wa zamani wa Ulinzi wa Mexico, Salvador Cienfuegos Zepeda, amezuiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Los Angeles katika jimbo la California, Waziri wa Mambo ya nje wa Mexico Marcelo Ebrard alisema hapo juzi.

Ebrard aliandika katika akaunti yake rasmi ya Twitter kwamba aliarifiwa juu ya kuzuiliwa na Balozi wa Marekani nchini Mexico Christopher Landau, akiongeza kuwa nae Balozi wa Mexico huko Los Angeles atakuwa akimjulisha mashtaka hayo “katika masaa machache yajayo.”

“Tutatoa msaada wa kibalozi ambao yeye (Cienfuegos) anastahili,” Ebrard aliandika.Kufikia sasa, hakukuwa na uthibitisho kutoka kwa maafisa wa Marekani juu ya kuzuiliwa kwake.

Cienfuegos aliwahi kuwa waziri wa ulinzi wa Mexico mnamo mwaka 2012-2018 chini ya Rais Enrique Pena Nieto wa wakati huo.