NA KHAMISUU ABDALLAH

KIJANA mwenye umri wa miaka 30 amefikishwa katika mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe mbele ya Hakimu Subeit wa mahakama hiyo akikabiliwa na mashitaka matano.

Mshitakiwa huyo ambae ni mkaazi wa Magomeni wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka yake na Mwendesha Mashitaka Wakili wa serikali kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Soud Said.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kosa la kwanza alilopatikana nalo mshitakiwa huyo ni kushindwa kuvaa sare ya udereva kinyume na kifungu cha 60 (1) (g) (2) sheria ndogo ndogo za magari ya biashara chini ya kifungu cha 80 cha sheria namba 7 ya mwaka 2003 sheria za Zanzibar.

Soud alidai kuwa Septemba 9, mwaka huu saa 12:46 jioni huko Amani kwenye mzunguko wa barabara mshitakiwa huyo akiwa dereva wa gari yenye namba za usajili Z. 731 CW inayoenda njia 516 akitokea Nyerere skuli kuelekea Darajabovu alipatikana akiwa hakuvaa sare ya udereva kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Kosa la pili alilopatikana nalo mshitakiwa huyo ni kushindwa kusimama aliposomamishwa na askari polisi aliyekuwepo kazini kinyume na kifungu cha

Hakimu alidaiwa kuwa siku hiyo hiyo katika maeneo hayo alisimamishwa na askari WP 6171 PC Msemo akiwa amevaa sare za polisi akiwa kazini na kukataa kusimama.

Makosa mengine aliyopatikana nayo mshitakiwa huyo ni kuweka gari sehemu hatarishi kinyume na kifungu cha 143 cha sheria namba 7 ya mwaka 2003 na kushindwa kutoa anuani kinyume na kifungu 165 (1) na kinyume na kifungu cha 201 (1) cha sheria namba 7 ya mwaka 2003 sheria za Zanzibar.

Mwendesha Mashitaka Soud, alidai kuwa mshitakiwa alidaiwa kusimamisha gari yake kwenye mpindo wa barabara na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara hiyo na aliposimamishwa alishindwa kutoa anuani kwa askari Msemo akiwa amevaa sare za polisi akiwa kazini.