NA ZUHURA JUMA, PEMBA

TIMU ya Alpari ya Kifumbikai imeibuka ubingwa katika fainali ya shindano la Dande Cup Wilaya ya Wete baada ya kuifunga timu ya Al-kumas ya Kibokoni bao 1-0.

Baada ya timu hizo kuingia uwanjani majira ya saa 10:00 katika uwanja wa Utaani, zilipambana vikali, ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyofunga.

Timu hizo mbili wakati zikiwania kombe la mbuzi, katika kipindi cha pili cha mchezo huo timu ya Alpari iliibuka na ushindi kwa kupata bao lake kutoka kwa mchezaji wake Nassor Khamis Ali (Kamara) mnamo dakika ya 60.

Timu ya Al-pari ilipatiwa zawadi ya kombe, mbuzi wawili na mipira miwili na timu ya Al-kumas ilizawadiwa mbuzi mmoja na mipira miwili.