BOGOTA,COLOMBIA

SHIRIKA la utetezi wa haki za binaadamu duniani, Amnesty International, limesema vitisho vya mara kwa mara, mashambulzi na mauwaji yanayowalenga wanaharakati nchini Colombia vinauweka wazi uwezo mdogo wa serikali ya taifa hilo katika kuwalinda watetezi wa haki za binaadamu.

Mkurugenzi wa shirikia hilo katika eneo la Marekani ya Kusini, Erika Guevara-Rosas, alisema hali hiyo inaweza kufikia kikomo endapo Serikali za mataifa hayo zitafanikiwa kufanikisha haki na usawa na kudhibiti biashara haramu.

Alisema migogoro ya makundi yenye kujihami na silaha imekuwa kama maisha ya kawaida kwa wakaazi wengi wa maeneo hayo.

Idadi kubwa ya viongozi katika ngazi ya kijamii na wanaharakati, kwa idadi tofauti ilitajwa kupata vitisho na wengine kupoteza maisha kila mwaka.