LONDON, UINGEREZA

SHIRIKA la kimataifa la haki za binadaamu la Amnesty International limelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka dhidi ya Myanmar.

Shirika hilo limesema si vyema kuchukua hatua kabla ya mahakama ya jinai ya Kimataifa halijafanya hivyo, kutokana na kuwepo kwa ushahidi wa dhuluma za kiutu zilizofanywa na wanajeshi wa nchi hiyo.

Shirika hilo limeeleza kuwa wanajeshi nchini humo wamefanya unyama mkubwa ikiwemo kuwaua watu kwa kuwafyatulia risasi kiholela.

Myanmar kijiji

Amnesty ilisema kwamba ushahidi wa picha na video uliopatikana na kundi hilo unaonyesha wanajeshi wa Myanmar “kupuuza kabisa mateso ya raia” katika maeneo ya mapigano.

Matukio kadhaa yanayohusu raia waliojeruhiwa au kuuawa na mabomu ya ardhini na mabomu ya kawaida, yameripotiwa katika majimbo ya Chin na Rakhine katika wiki za hivi karibuni.

Inasemekana kuwa hakuna dalili zozote za mzozo kati ya Jeshi la Arakan na wanajeshi wa Myanmar lakini wanaendelea kuumia ni raia.