LONDON, England

HOUSSEM AOUAR  amesema ana furaha kuwepo Lyon klabu yake ya utotoni kwa msimu mwengine, baada ya Arsenal kushindwa kumsajili.

Mikel Arteta aliwataka  Aouar wa Lyon na Thomas Partey kutoka Atletico Madrid ambao aliwapa nafasi kubwa ya kuwasajili viungo hao mwanzo wa msimu, lakini beki wa kati wa Lille, Gabriel Magalhaes alikuwa mchezaji pekee aliyejiunga na Arsenal zikiwa zimesalia saa chache kufungwa dirisha la usajili.

 Ingawaje, Arsenal ilifanikiwa kumpata Partey baada ya kutoa pauni milioni 45  kutoka Atletico Madrid siku ya mwisho, na Mghana huyo anaweza kucheza mara ya kwanza wakati timu yake itakaposafiri kwenda Manchester City wiki ijayo.

Arsenal wanatarajiwa kurudi  tena  kumsajili Aouar katika kipindi cha uhamisho cha Januari au msimu ujao wa joto, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ana anasisitiza bado ana hamu kubwa ya kuichezea Lyon, timu ambayo amekuwa nayo tangu akiwa na umri wa miaka 11.

Aouar ameongeza: ‘Nina furaha kukaa Lyon. ‘Ni mji yangu, ni klabu yangu: ni fahari kubwa kumwakilisha OL. ‘Haikuwa lazima Arsenal au kitu kingine chochote, ingawa mwishowe ilikuwa hivyo. “Nilipaswa kufanya uamuzi na ninafurahi kukaa hapa.”

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Kevin Campbell ana imani Aouar atakuwa  kwenye rada za Arteta na Edu’ baada ya klabu hiyo kumkosa msimu huu wa joto.