ZASPOTI
KLABU za soka za APR na AS Kigali zimeruhusiwa kuanza mazoezi, Wizara ya Michezo ya Rwanda, imetangaza.
Maendeleo hayo, kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara ya michezo, inakuja baada ya timu zote mbili kutii kikamilifu hatua za kuzuia virusi vya ‘corona’ ambazo kati ya nyengine ni pamoja na kuwapima wachezaji wote na wafanyakazi.
Kwa kuongezea, washiriki wote wa timu husika wanapaswa kukaa pamoja na harakati yoyote isiyo ya dharura nje ya kambi inachukuliwa kama ukiukaji wa miongozo ya kinga.
Mabingwa APR watatumia uwanja wa nyasi bandia wa Shyorongi kama kituo chao cha mazoezi, wakati AS Kigali watakuwa wakifanya mazoezi kwenye uwanja wa Kigali.
“Ninachukua fursa hii kuitaka taasisi yako kusimamia utekelezaji wa miongozo na kuwasilisha ripoti hiyo kla wiki mbili kwa Wizara ya Michezo”, Didier Shema Maboko, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, alisema, katika barua kwenda kwa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa).
APR itawakilisha Rwanda kwenye Ligi ya Mabingwa ya Caf ya 2020/21, wakati AS Kigali itashiriki Kombe la Shirikisho.(Goal).