LONDON, England

MENEJA wa Arsenal Mikel Arteta amesema kufungwa bao 1-0 na Leicester City kumeharibu mipango yao.

Washika bunduki  hao walicheza vizuri zaidi katika kipindi cha kwanza, lakini walishindwa kupata bao.

Mfaransa alifanikiwa kupata bao lakini lilikataliwa baada ya Granit Xhaka alikuwa kwenye nafasi ya kuotea.

Arteta alikosoa uamuzi wa mwamuzi wa kukata bao la Lacazette na anasema hajui ‘jinsi bao hilo lilivyokataliwa.

 ‘Nadhani kipindi cha kwanza tulikuwa na mchezo mzuri ‘ alisema Arteta. ‘Tumetengeneza nafasi za kutosha kwenda mbele. Tulifunga bao ambalo sijui ni jinsi gani lilikataliwa.