KIGALI, Rwanda
AS Kigali wameripotiwa kukubali mpango wa kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Rwanda, Abeddy Biramahire kutoka timu ya Buildcon FC ya Zambia kuelekea msimu ujao wa 2020/21.
Biramahire imekuwa ikifanya mazungumzo na Rayon Sports, lakini, AS Kigali tangu wakati huo imeibuka katika msimamo wa kupata huduma za mshambuliaji huyo wakati klabu ikijiandaa kwenye Kombe la Shirikisho la Caf.


Kuhamia Ryon kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ilifikiriwa kukaribia makubaliano yaliyofanyika kwa muda, lakini, tatizo la kifedha na kushindwa kwa utawala wa hivi karibuni huko ‘Blues’ kunaonekana kuzamisha uhamisho huo.
Kabla ya kujiunga na Buildcon mnamo Julai 2019, Biramahire alichezea Mukura ya Ligi Kuu ya Rwanda kwa miezi sita na alikuwa ameshiriki na klabu ya Sfaxien ya Tunisia tangu Septemba 2018.


Katibu Mkuu wa AS Kigali, Francis Gasana, alithibitisha kuwa pande hizo mbili zilikuwa katika ‘mazungumzo ya hali ya juu’ lakini makubaliano ya mwisho hayajafikiwa.
“Tumekuwa kwenye mazungumzo kwa muda na maendeleo hadi sasa yanatia moyo,” alisema. “Tunahitaji mshambuliaji anayeweza kucheza na Alex Orotomal, lakini, ambaye pia ana uwezo wa kuchukua nafasi yake wakati Anahitajika, Biramahire ni mgombea mzuri wa jukumu hilo, na tunatarajia hivi karibuni mpango utafikiwa.”


Biramahire alikuwa sehemu ya kikosi cha Amavubi kilichoshiriki mashindano ya fainali za Mashindano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) mwaka 2018 nchini Morocco.(Goal).