LONDON, England
NAHODHA wa Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang, amejiondoa katika timu ya taifa ya Gabon, sababu kubwa ikiwa ni maumivu ya kifundo cha mguu aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Sheffield United wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa kocha wa timu ya taifa ya Gabon, Patrice Neveu, alisema: “Aubameyang hatakuwa sehemu ya timu katika mchezo wetu wa kimataifa dhidi ya Benin.”Kama kocha nasikitika kumkosa mchezaji huyu kikosin, lakini hamna jinsi”.

Aubameyang hajasafiri na timu kwenda Lisbon nchini Ureno, madaktari wa timu wamethibitisha hawezi kucheza kwa sasa, kwa kuwa mechi hiyo itachezwa kesho.(Goal).