NA SAIDA ISSA, DODOMA

BARAZA la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limelaani vikali kauli iliyotolewa na Sheikh Issa Ponda kwamba waislamu nchini wamekubaliana kumpigia kura mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kwa chama cha CHADEMA, Tundu Lissu.

Itakumbukwa kuwa mnamo Oktoba 17 mwaka mwaka huu katika mkutano wa kampeni wa kumnadi Lissu uliofanyika katika uwanja wa skuli ya Msingi Uhuru jijini Dodoma, Sheikh Ponda alipewa nafasi ya kuzungumza ambapo alinukuliwa akisema kwamba waislamu wamekubaliana kwamba kura zote ni kwa Lissu

“…Hii ni kauli ya kwake yeye mwenyewe hakuna muislamu popote wala sehemu yoyote wala kikao chochote walichokaa na kukubaliana kwamba eti wakipe kura chama fulani au mgombea fulani kama alivyoeleza Ponda…

“…Haya maneno yapuuzwe sio sahihi ni maneno ambayo mtu ameyazunguza kwa maslahi yake kwa hiyo maneno haya yanaashiria uvunjifu wa amani yale maneno anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria kwa sababu moja kwa moja anahamasisha watu vurugu ama uvunjifu wa amani kwa sababu kuna maisha baada ya uchaguzi na kuna kushinda na kushindwa,” alisema.

Sheikh Rajabu alisema wanakemea tamko hilo na kwamba msemaji wa mambo ya BAKWATA ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Zubeir.

“Halazimishwi mtu yoyote kuwa upande wa chama fulani yale maneno tunarudia kusema yale maneno yapuuzwe kwa sababu msemaji wa BAKWATA ni Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir na wala siyo Sheikh Ponda kwani hajulikani ni kiongozi wa Taasisi gani au ni mwalimu wa madrasa gani sisi hatumtambui”, alisema.

Alisema kuwa hivi karibuni   Baraza la Masheik Mkoa wa Dodoma lilikaa kikao ambapo   ajenda walizokubaliana ni kuwakumbusha viongozi wa dini wajibu wao wakati wa kipindi hichi cha kampeni.

“Lakini pia mbaya zaidi katika ajenda ambazo tumekubaliana ni kuwakumbusha viongozi wa dini wajibu wao kwa sababu toka tuanze kampeni hizi za kuingia katika uchaguzi kumekuwa na maneno ya viongozi wa dini ambayo yanaleta ukakasi.

“Kutokujihusisha na kupigia kampeni chama chochote bali kila kiongozi ana utashi na chama anachokitaka yeye.